>>’NATEGEMEA
TUTAPATA NAFASI YA KUCHEZA 11 DHIDI YA 11!’
UEFA
CHAMPIONZ LIGI
Raundi
ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO
[Kwenye
Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumanne
Machi 11
[Saa
za Bongo]
22:45
Bayern Munich v Arsenal FC [2-0]
22:45
Atletico de Madrid v AC Milan [1-0]
++++++++++++++++++++++++++++++++++
![]() |
Meneja wa Arsenal Arsène Wenger |
Akiongea
kabla ya Mechi yao ya Marudiano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI,UCL, ya Usiku huu huko
Allianz Arena, Munich dhidi ya Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich, Arsène Wenger
ametaka kuwepo na haki kutoka kwa Refa.
Refa
wa Mechi hii ya Leo kati ya Arsenal na Bayern ni Svein Oddvar Moen, mwenye Miaka
35, na anaetoka Norway.
Wenger
alikumbushia walivyokuwa wakionewa na Marefa kwenye Mechi zao za nyuma za UCL.
Meneja
huyo awa Arsenal alikumbushia jinsi Kipa wake Wojciech Szczesny apolitolewa nje
kwa Kadi Nyekundu walipofungwa 2-0 huko Emirates katika Mechi ya kwanza
na Bayern Wiki 3 zilizopita na pia kuyataja matukio ya nyuma kwenye UCL ambapo
Mwaka 2006 kwenye Fainali na Barcelona Kipa wao Jens Lehmann alitolewa nje kwa
Kadi Nyekundu na pia Mwaka 2011 huko Nou Camp na Barcelona jinsi Robin van Persie
alivyopewa Kadi ya Njano ya Pili kwa kucheza Mpira baada Filimbi kulia na
kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Wenger
amesema: “Tumecheza mara kadhaa Ulaya tukiwa Mtu 10! Safari hii natumaini haki
itatendeka na tutacheza 11 dhidi ya 11 mpaka mwisho!”
Kwenye
Mechi ya Leo, Wenger amesema Kieran Gibbs atakuwa nje akiwa na maumivu ya Enka
na atalazimika kumchezesha Thomas Vermaelen kwenye Nafasi ya Fulbeki wa Kushoto
kwa vile Nacho Monreal nae pia ni Majeruhi.
Hata
hivyo, Wenger ametamka kuwa wanao uwezo wa kuwafunga Bayern Munich kwao Allianz
Arena baada ya kufanya hivyo Msimu uliopita kwenye hatua kama hii ya UCL
walipofungwa 3-1 Emirates na kuichapa Bayern 2-0 katika Marudiano na kutolewa
kwa Magoli ya Ugenini.
Amesema:
“Tumeshawahi kushinda hapa kabla hivyo tunajua tunaweza kufanya tena. Ingawa Takwimu
zinatupinga lakini tulifanya Mwaka 2003 tulipoishinda Inter Milan 5-1 San
Siro!”
UEFA
CHAMPIONZ LIGI
Raundi
ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO
[Kwenye
Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
[Saa
za Bongo]
Jumatano
Machi 12
22:45
FC Barcelona v Manchester City [2-0]
22:45
Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen [4-0]
Jumanne
Machi 18
22:45
Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45
Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]
Jumatano
Machi 19
22:45
BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45
Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]
No comments:
Post a Comment