VPL-LIGI KUU VODACOM
RATIBA:
Jumamosi
Machi 15
Azam
FC v Coastal Union
Mtibwa
Sugar v Yanga
Kagera
Sugar v Tanzania Prisons
Jumatano
Machi 19
Yanga
v Azam FC
+++++++++++++++++++++++
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Machi
14, 2014
Klabu
ya Simba itafanya mkutano wa wanachama wake Jumapili (Machi 16 mwaka huu) kwa
ajili ya kuifanyia marekebisho Katiba yao.
Nachukua
fursa hii kuwatakia kila la kheri katika mkutano huo ambao ni muhimu katika
kuhakikisha klabu yao inapiga hatua katika maendeleo ya mpira wa miguu na
ustawi wake kwa ujumla.
Hata
hivyo, nawakumbusha viongozi na wanachama wa klabu ya Simba kuwa marekebisho
hayo ni lazima yafanyike kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na maelekezo ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Afrika (CAF) na Tanzania
(TFF).
Aidha
waraka wa TFF kwa wanachama wake wa Februari 7 mwaka huu uzingatiwe kikamilifu
katika marekebisho hayo.
TFF
inawatakia wanachama wa Simba mkutano mwema, na inawakumbusha wazingatie
umuhimu wa kudumisha amani na maelewano katika klabu yao.
Jamal
Malinzi
Rais
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
SEMINA YA WAAMUZI YAANZA DAR
Semina
ya siku mbili kwa waamuzi wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) na wale wa ngazi ya juu nchini (elite) kwa robo ya kwanza ya mwaka
huu inaanza kesho (Machi 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi
na waamuzi wasaidizi 22 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanashiriki katika
semina hiyo ambayo pia itahusisha mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness
test), na itamalizika keshokutwa (Machi 16 mwaka huu).
Baadhi
ya waamuzi hao ni Charles Simon kutoka Dodoma, Dalila Jafari (Zanzibar),
Ferdinand Chacha (Mwanza), Hamis Chang’walu (Dar es Salaam), Helen Mduma (Dar
es Salaam), Israel Mujuni (Dar es Salaam), Issa Vuai (Zanzibar), Janeth Balama
(Iringa) na Jesse Erasmo (Morogoro).
John
Kanyenye (Mbeya), Jonesia Rukyaa (Bukoba), Josephat Bulali (Zanzibar), Lulu
Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mfaume Nassoro (Zanzibar),
Mohamed Mkono (Tanga), Mwanahija Makame (Zanzibar), Ngaza Kinduli (Zanzibar),
Ramadhan Ibada (Zanzibar) na Waziri Sheha (Zanzibar).
YANGA
KUIVAA MTIBWA SUGAR VPL
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Machi 15 mwaka huu) kwa mechi tatu
ambapo mabingwa watetezi Yanga wataumana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro.
Nao
vinara wa ligi hiyo, Azam wanaikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi
itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mechi
nyingine itachezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwa kuwakutanisha wenyeji
Kagera Sugar dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya.
WATANZANIA WATANO WAKWAA UKAMISHNA CAF
Watanzania
watano wameteuliwa kuingia kwenye jopo la makamishna watakaosimamia mechi
mbalimbali za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa mwaka 2014 hadi
2016.
Kwa
mujibu wa orodha iliyotumwa na CAF kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Watanzania hao ni Alfred Kishongole Rwiza wa Mwanza na Hafidh Ali Tahir
wa Zanzibar ambao wamerejeshwa tena kwenye jopo hilo.
Rwiza
na Tahir ambao ni waamuzi wastaafu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) na wakufunzi wa uamuzi walikuwepo kwenye jopo lililopita la 2012 hadi
2014.
Makamishna
wapya kwa upande wa wanawake ni Elizabeth Mwanguku Kalinga wa Mbeya na
Isabellah Hussein Kapera wa Dar es Salaam. Kamishna mwingine mpya kwa upande wa
wanaume ni Muhsin Ali Rajab kutoka Zanzibar.
Wakati
huo huo, CAF imeandaa semina kwa makamishna wanaume itakayofanyika jijini
Cairo, Misri kuanzia Aprili 3 hadi 4 mwaka huu.
Watoa
mada kwenye semina hiyo ya siku mbili ni Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani,
Mkurugenzi wa Mashindano wa CAF, Shereen Arafa na Naibu Mkurugenzi wa
Mashindano wa CAF, Khaled Nassar.
Wengine
ni Meneja wa Waamuzi wa CAF, Eddy Maillet, Mkurugenzi wa Habari wa CAF, Junior
Binyam, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Mawasiliano wa CAF, Tarek el Deeb na
Mkurugenzi wa Masoko na Televisheni wa CAF, Amr Shaheen.
Boniface
Wambura Mgoyo
Media
and Communications Officer
Tanzania
Football Federation (TFF)
No comments:
Post a Comment